Kila siku tunasikia matukio ya wizi, uharibifu na uvunjaji wa nyumba au ofisi. Njia bora ya kuimarisha usalama ni kufunga CCTV Camera. Lakini tatizo linalowakumba wengi ni: “Ni CCTV ipi bora kuchagua kwa nyumba au ofisi yangu?”
Hapa tumekuandalia mwongozo rahisi utakusaidia kufanya uamuzi sahihi.
🔎 Mambo ya Kuzingatia Unapochagua CCTV Camera
1. Ubora wa Picha (Resolution)
Kwa nyumba: CCTV yenye HD (720p au 1080p) inatosha.
Kwa ofisi au biashara kubwa: Tumia Full HD au 4K kwa picha safi zaidi.
2. Aina ya Camera
•Dome Camera – Nzuri kwa ndani (indoor), inachanganyika na mazingira bila kuonekana sana.
•Bullet Camera – Bora kwa nje (outdoor), inafaa kwa ufuatiliaji wa mbali.
•PTZ (Pan-Tilt-Zoom) – Ina uwezo wa kuzunguka na kukuza picha, inafaa kwa maeneo makubwa.
•Wi-Fi / Smart Camera – Haziitaji wiring nyingi, unaweza kuziunganisha moja kwa moja na simu.
3. Usiku na Mwangaza Hafifu (Night Vision)
Hakikisha camera ina infrared (IR) au full color night vision ili kurekodi vizuri usiku.
4. Hifadhi ya Video (Storage)
- DVR/NVR na Hard Disk – Inafaa kwa mifumo yenye camera nyingi.
- Cloud Storage – Inawezesha kuangalia video popote ulipo.
5. Uhimilivu wa Mazingira
Kwa kamera za nje, hakikisha zina kinga ya maji na jua (weatherproof).
💡 Ushauri Maalum
>Kwa nyumba ndogo: Mfumo wa 4 hadi 6 cameras unatosha.
>Kwa ofisi ndogo: Angalau 4 hadi 8 cameras.
>Kwa biashara kubwa / hoteli: 8 hadi 16 cameras au zaidi, kulingana na ukubwa.
✅ Kwa Nini Uchague Mustapha Madish Installers?
- Tunakushauri kulingana na mahitaji yako halisi.
- Tunatoa vifaa vya asili kutoka kwa brands bora duniani.
- Huduma zetu zinaambatana na ufungaji wa kitaalamu na udhamini.
-Unaweza kuangalia kazi zako zote kupitia simu yako (Remote Viewing).
📞 Wasiliana Nasi Leo
👉 WhatsApp / Simu: +255 777 139 413 / 775 949 413
👉 Email: mustaphamadishinstallers@gmail.com
Linda usalama wa familia na biashara yako kwa kuchagua mfumo bora wa CCTV kutoka Mustapha Madish Installers.
